Al-Baqara 2:67
البقرةوَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦٓ إِنَّ ٱللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا۟ بَقَرَةً ۖ قَالُوٓا۟ أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا ۖ قَالَ أَعُوذُ بِٱللَّهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ ٱلْجَـٰهِلِينَ
Na Musa alipowaambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje ng'ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema: "A'udhu billah (Najikinga kwa Mwenyezi Mungu) nisiwe miongoni mwa wajinga."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Musa alipo waambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje Ng'ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema: Audhubil lahi! Najikinga kwa Mwenyezi Mungu nisiwe miongoni mwa wajinga. [67]
[67] Na kumbukeni pale alipo uliwa mtu na asijuulikane muuwaji, Musa akawaambia watu wake: Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje Ng'ombe ili iwe ndio ufunguo wa kumgundua muuwaji. Lakini wakaona hayo ni mageni, baina ya yale mauwaji na kumchinja ng'ombe. Wakasema: Unatufanyia maskhara wewe Musa? Yeye akawajibu: Mimi najilinda kwa Mwenyezi Mungu asinipatilize kwa kuwa katika wajinga wanao wadhihaki waja wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbukeni, enyi wana wa Isrãîl, makosa ya mababu zenu, ushindani wao mwingi na kujadiliana kwao na Mûsã, rehema na amani zimshukie, pindi alipowaambia, “Hakika Allah Mtukufu Anawaamuru mchinje ng’ombe.” Wakasema, wakiwa na kiburi, “Unatufanyia mzaha na kutuchezea?” Mûsã akawajibu, “Ninajilinda kwa Allah Mtukufu nisiwe ni miongoni mwa wanaofanya stihizai.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net