Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 67

وَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦٓ إِنَّ ٱللَّهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تَذْبَحُوا۟ بَقَرَةً ۖ قَالُوٓا۟ أَتَتَّخِذُنَا هُزُوًا ۖ قَالَ أَعُوذُ بِٱللَّهِ أَنْ أَكُونَ مِنَ ٱلْجَـٰهِلِينَ 67

(67) Yani: Na kumbukeni yale yaliyowapata pamoja na Musa wakati mlipomuua mtu; hivyo mkahitilafiana kwa hilo juu ya muuaji wake mpaka jambo hilo likawa kubwa baina yenu, na ikakaribia sana - lau kuwa si Mwenyezi Mungu kuwabainishia -, kutokea uovu mkubwa baina yenu. Basi Musa akawaambia katika kubainisha muuaji: Mchinjeni ng'ombe (wa kike). Na ilikuwa wajibu kuharakisha kutekeleza amri yake na kutoipinga. Lakini wao wakakataa isipokuwa kuipinga, na wakasema: "Je, unatufanyia mzaha?" Nabii wa Mwenyezi Mungu akasema: "Audhu billahi (Najikinga kwa Mwenyezi Mungu) nisiwe miongoni mwa wajinga." Kwa maana, mjinga ni yule anayesema maneno yasiyokuwa na faida. Naye ndiye huwafanyia watu mzaha. Na ama mwenye akili timamu, yeye anaona kuwa moja ya makosa makubwa ya kidini na kiakili ni kumfanyia mzaha yule ambaye ni mwanadamu kama yeye. Na ikiwa ameboreshwa juu yake, basi kuboreshwa kwake huko kunamlazimu amshukuru Mola wake Mlezi, na awarehemu waja wake. Na Musa alipowaambia hayo, wakajua kwamba hilo ni kweli, hivyo wakasema: