Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 66

Al-Baqara 2:66

البقرة

فَجَعَلْنَـٰهَا نَكَـٰلًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهَا وَمَا خَلْفَهَا وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ

Maana

Kwa hivyo tukayafanya hayo kuwa onyo kwa wale waliokuwa katika zama zao na waliokuja baada yao, na mawaidha kwa wacha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa hivyo tukayafanya hayo kuwa onyo kwa wale walio kuwa katika zama zao na walio kuja baada yao, na mawaidha kwa wachamngu. [66]

[66] Mwenyezi Mungu ameifanya hali yao namna hii waliyo ifikia ili iwe ni kama funzo na onyo kwa wengineo, wasitende kitendo kama hichi. Ameyafanya haya ili yazingatiwe na watu wa nyakati zao na watakao kuja baada yao, kama tulivyo yafanya kuwa ni mawaidha kwa wale wanao mcha Mola wao Mlezi, kwani wao ndio wanao nafiika kwa maonyo ya mawaidha na mazingatio.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tukakifanya kijiji hicho ni mazingatio kwa watu wa vijiji vya karibu ambao itawafikia habari yake na vituko vilivyotokea huko, na ni mazingatio kwa mwenye kufanya madhambi kama hayo baada yake. Na pia tulikifanya ni mawaidha kwa watu wema, wapate kujua kuwa wao wako kwenye haki, ili wasimame imara juu yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net