Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 65

Al-Baqara 2:65

البقرة

وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ ٱلَّذِينَ ٱعْتَدَوْا۟ مِنكُمْ فِى ٱلسَّبْتِ فَقُلْنَا لَهُمْ كُونُوا۟ قِرَدَةً خَـٰسِـِٔينَ

Maana

Na hakika mlikwishayajua ya wale miongoni mwenu waliopindukia mipaka kuhusu Sabato (siku ya Jumamosi) na tukawaambia: Kuweni manyani mliodhalilika.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika mlikwisha yajua ya wale miongoni mwenu walio ivunja Sabato, (siku ya mapumziko, Jumaa Mosi) na tukawaambia: Kuweni manyani wadhalilifu. [65]

[65] Na nyinyi bila ya shaka mliwajua wale walio pindukia mipaka katika siku ya Sabato, siku ya ibada na mapumziko, siku ya Jumaamosi. Pale walipo kwenda kuvua samaki siku hiyo na ilhali siku hiyo ilikuwa imetengwa iwe ni siku ya mapumziko na siku kuu, na kufanya kazi siku hiyo ilikatazwa. Mwenyezi Mungu alizipotoa nyoyo za wakosefu wale, wakawa kama manyani katika pumbao lao na matamanio yao. Tukawaweka mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu, wakifukuzwa kama mijibwa, watu hawataki kukaa nao, na wanawanyanyapaa kuchanganyika nao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika mlijua, enyi kongamano la Mayahudi na Wanaswara, adhabu iliyowapata mababu zenu waliopita, watu wa kijiji kilichoasi amri ya Allah Mtukufu katika yale aliyowachukulia ahadi ya kuitukuza Siku ya Jumamosi. Wakafanya hila ya kuvua samaki siku ya Jumamosi kwa kuweka mitego na kufukua mashimo. Walipofanya hivyo, Allah Mtukufu aliwageuza kuwa manyani wenye kudharauliwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net