Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 64

Al-Baqara 2:64

البقرة

ثُمَّ تَوَلَّيْتُم مِّنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ ۖ فَلَوْلَا فَضْلُ ٱللَّهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُۥ لَكُنتُم مِّنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ

Maana

Kisha mligeuka baada ya haya. Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema zake, mngelikuwa miongoni mwa wenye kupata hasara.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha mligeuka baada ya haya. Na lau kuwa si fadhila za Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema zake, mngeli kuwa miongoni mwa wenye kukhasirika. [64]

[64] Tena baada ya hayo yote mkageuka. Na lau kuwa si fadhila na rehema ya Mwenyezi Mungu juu yenu kuiakhirisha adhabu kwenu mngeli kwisha kuwa miongoni walio potea na kuangamia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha mlienda kinyume na mkaasi mara nyingine, baada ya kuchukuwa ahadi ya mkazo na kunyanyuliwa jabali, kama desturi yenu daima. Na lau si wema wa Allah Mtukufu na rehema Yake kuikubali toba yenu na kuyasamehe makosa yenu, mungalikuwa ni wenye hasara ya duniani na ya Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net