Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 53

Al-Baqara 2:53

البقرة

وَإِذْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْفُرْقَانَ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ

Maana

Na tulipompa Musa Kitabu na pambanuo ili mpate kuongoka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tulipo mpa Musa Kitabu na pambanuo ili mpate kuongoka. [53]

[53] Na kumbukeni tulipo kuneemesheni kwa kukumteremshia Nabii wenu Musa Kitabu chetu Taurati, Kitabu ambacho kinafarikisha baina ya Haki na baat'ili, na kinabainisha baina ya Halali na Haramu, ili mpate kupata uwongozi kwa nuru yake na muongoke kutokana na upotovu kwa kuzingatia yaliyomo ndani yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbukeni neema Yetu juu yenu, tulipompa Mûsã Kitabu chenye kupambanua baina ya haki na batili- nacho ni Taurati- ili muongoke na mtoke kwenye upotevu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net