Al-Baqara 2:54
البقرةوَإِذْ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوْمِهِۦ يَـٰقَوْمِ إِنَّكُمْ ظَلَمْتُمْ أَنفُسَكُم بِٱتِّخَاذِكُمُ ٱلْعِجْلَ فَتُوبُوٓا۟ إِلَىٰ بَارِئِكُمْ فَٱقْتُلُوٓا۟ أَنفُسَكُمْ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ عِندَ بَارِئِكُمْ فَتَابَ عَلَيْكُمْ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ
Na Musa alipowaambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmezidhulumu nafsi zenu kwa kuchukua kwenu ndama (kumuabudu). Basi tubuni kwa Muumba wenu na ziueni nafsi zenu. Haya ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu. Naye akapokea toba yenu. Hakika Yeye ndiye apokeaye toba mno, Mwenye kurehemu zaidi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmezidhulumu nafsi zenu kwa kuchukua kwenu ndama (kumuabudu). Basi tubuni kwa Muumba wenu na ziueni nafsi zenu. Haya ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu. Naye akapokea toba yenu. Hakika Yeye ndiye apokeaye toba na Mwenye kurehemu. [54]
[54] Ikumbukeni siku alipo kwambieni Mtume wenu Musa: Enyi watu wangu! Mmejidhulumu kwa kumchukua ndama wa Saamiriyu mkamuabudu. Basi tubuni kwa Mola wenu aliye kuumbeni kabla hamjawa kitu, kwa kuzighadhibikia nafsi zenu ovu zenye kuamrisha maovu, na zifanyeni hizo nafsi ziwe nyonge, ili mpate nafsi mpya zilio safi. Mwenyezi Mungu alikusaidieni kwa hayo na akakuwezesheni mkaweza, na hiyo ni kheri itokayo kwa Muumba wenu. Na haya ni kabla ya kutubu kwenu, Naye akakusameheni. Kwani Yeye ni mwingi wa kukubali toba kwa waja wake, na mwingi wa kuwarehemu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kumbukeni neema Zetu kwenu, aliposema Mûsã kuwaambia watu wake, “Hakika nyinyi mlijidhulumu nafsi zenu kwa kumfanya ndama ni mungu, basi tubieni kwa Muumba wenu kwa kuuana nyinyi kwa nyinyi. Kufanya hivyo ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu kuliko kukaa milele Motoni.” Na nyinyi mlifuata amri hiyo, ndipo Allah Mtukufu Akawafanyia wema kwa kuikubali toba yenu. Hakika Yeye, Aliyetukuka, Ndiye Mwingi wa kukubali toba za wenye kutubia miongoni mwa waja wake na Ndiye Mwenye kuwarehemu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net