Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 52

Al-Baqara 2:52

البقرة

ثُمَّ عَفَوْنَا عَنكُم مِّنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Maana

Kisha tukakusameheni baada ya hayo, ili mpate kushukuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukakusameheni baada ya hayo, ili mpate kushukuru. [52]

[52] Kisha tukakusameheni na tukaifuta adhabu yenu mlipo tubu na mkapata msamaha kwa dhambi zenu, ili mpate kumshukuru Mola Mlezi wenu kwa huko kufuta kwake makosa yenu, na kusamehe kwake, na fadhila zake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukawasamehe kitendo hiki kibaya, tukakubali toba yenu baada ya kurudi Mûsã kwa kutarajia kuwa mtamshukuru Allah Mtukufu kwa neema Zake na fadhila Zake juu yenu, na hamtaendelea kwenye ukafiri na uasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net