Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 51

Al-Baqara 2:51

البقرة

وَإِذْ وَٰعَدْنَا مُوسَىٰٓ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً ثُمَّ ٱتَّخَذْتُمُ ٱلْعِجْلَ مِنۢ بَعْدِهِۦ وَأَنتُمْ ظَـٰلِمُونَ

Maana

Na tulipomuahidi Musa usiku arubaini, kisha mkamchukua ndama (mkamuabudu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tulipo muahidi Musa masiku arubaini, kisha mkachukua ndama (mkamuabudu) baada yake, na mkawa wenye kudhulumu. [51]

[51] Na kumbukeni wakati Mola wenu alipo agana na Musa muda wa masiku arubaini kwa ajili ya mazungumzo. Alipo kwenda walipo agana na akarejea alikukuteni mmekwisha geuka, na mkamfanya ndama aliye muunda Saamiriyu ndiye wa kuabudiwa. Mkawa kwa hivyo ni wenye kudhulumu kwa kumfanyia Mwenyezi Mungu aliye kuumbeni na kukuokoeni ana mshirika wake. ("Masiku" ni wingi wa Usiku. Wingi wa siku ni siku, kama ilivyo sahani, sabuni, silaha, sinia, sungura, saa. Ni makosa kwa Kiswahili kusema "masiku" kuwa ni wingi wa siku; "Masiku" ni wingi wa "Usiku". Kutumia "Masaa" kuwa ni wingi wa "Saa" ni makosa.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kumbukeni neema Yetu juu yenu, tulipompa Mûsã agizo la masiku arubaini la kuteremshiwa Taurati, iwe ni uongofu na nuru kwenu, na punde tu alipoondoka mlichukua fursa ya kuwa yeye hayupo kwa muda mchache, mkamfanya ndama, mliyomtengeneza kwa mikono yenu, kuwa ni mungu wenu wa kuabudiwa badala ya Allah Mtukufu. Huu ni ukanushaji Allah Mtukufu mbaya kabisa. Na nyinyi mlikuwa madhalimu kwa kumfanya ndama ni Mungu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net