Al-Baqara 2:31
البقرةوَعَلَّمَ ءَادَمَ ٱلْأَسْمَآءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى ٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ فَقَالَ أَنۢبِـُٔونِى بِأَسْمَآءِ هَـٰٓؤُلَآءِ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa nyinyi ni wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na akamfundisha Adam majina ya vitu vyote, kisha akaviweka mbele ya Malaika, na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli. [31]
[31] Na baada ya Mwenyezi Mungu kwisha kumuumba Adam na akamfundisha majina ya vitu vyote na sifa zao ili atue katika ardhi na anufaike navyo, aliwaletea hivyo vitu Malaika na akawaambia: Niambieni majina ya vitu hivi na sifa zao kama kweli nynyi ndivyo kama mnavyo dhani kuwa mnastahiki kupewa madaraka katika Ardhi, na kuwa hapana aliye bora kuliko nyinyi kwa sababu ya ut'iifu wenu na ibada zenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ili kubainisha utukufu wa Ãdam, Amani imshukiye, Allah Mtukufu Alimfundisha majina ya vitu vyote, kisha Akaviorodhesha hivyo vitu kwa Malaika na kuwaambia, “Niambieni majina ya vitu hivi vilivyoko, ikiwa nyinyi ni wakweli kwamba nyinyi mnastahiki zaidi uimarishaji wa ardhi kuliko wao.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net