Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 31

وَعَلَّمَ ءَادَمَ ٱلْأَسْمَآءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى ٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ فَقَالَ أَنۢبِـُٔونِى بِأَسْمَآءِ هَـٰٓؤُلَآءِ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ 31

Kisha, pale kauli ya Malaika, amani iwe juu yao, ilipokuwa inaashiria ubora wao juu ya huyo khalifa ambaye Mwenyezi Mungu atamweka katika ardhi, Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kuwabainishia katika ubora wa Adam. Ambao kwa ubora huo watajua ubora wake, na ukamilifu wa hekima na elimu ya Mwenyezi Mungu.

(31) Hivyo, “akamfundisha Adam majina yote.” Yani ya vitu vyote, yani namna vinavyoitwa, na akamfunza jina na maana yake, yani matamshi na maana, hata ukubwa wa neno kama vile ‘hili bakuli’, na udogo kama vile ‘kijibakuli’. “Kisha akaviweka,” yani aliweka hivyo vilivyotajwa “mbele ya Malaika” ili kuwajaribu, je wanavijua au la?" Na akasema: Niambieni majina ya hivi ikiwa mnasema kweli,” katika ile kauli yenu na dhana (firika) yenu kuwa nyinyi ni bora kuliko khalifa huyu.