Al-Baqara 2:30
البقرةوَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّى جَاعِلٌ فِى ٱلْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوٓا۟ أَتَجْعَلُ فِيهَا مَن يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّىٓ أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ
Na pale Mola wako Mlezi alipowaambia Malaika: 'Hakika Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi)', wakasema: Utaweka humo atakayefanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: 'Hakika Mimi nayajua msiyoyajua.'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo yajua. [30]
[30] Mwenyezi Mungu, Subhanahu, Aliye Takasika, amebainisha kuwa ni Yeye ndiye aliyempa uhai mtu, na akamweka duniani. Kisha amebainisha vile vile asli ya kumweka mwanaadamu na ujuzi aliyo mpa, na akakumbushwa hayo. Basi kumbuka, ewe Muhammad, neema nyingine ya Mola wako Mlezi kumpa mtu, nayo ni pale alipo waambia Malaika: Mimi nitajaalia awepo katika ardhi mfwatizi, ambaye nitamweka hapo, na nimpe madaraka, naye ni Adam na vizazi vyake. Mwenyezi Mungu atamweka kama Khalifa, au naibu wa kuimarisha dunia, na kutekeleza amri, na kuzitengeneza nafsi. Malaika wakauliza kutaka kujua nini siri ya hayo, wakasema: Je, utaweka katika Ardhi atakaye leta uharibifu humo kwa maasi, na atakaye mwaga damu kwa uadui na mauwaji kwa kufuata tabia yake ya matamanio, na ilhali sisi tunakutakasa na yasiyo laiki na utukufu wako, na tunasafisha kumbusho lako, na tunakutukuza? Mola wao Mlezi akajibu: Mimi ninajua maslaha ya hayo msiyo yajua nyinyi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kumbuka, ewe Mtume, Aliposema Mola wako kuwaambia Malaika, “Mimi nitawaweka watu kwenye ardhi, ili waiimarishe kwa kupishana: wakiondoka watu watakuja wengine baada yao.” Wakasema, “Ewe Mola wetu! Tufundishe na utuongoze, ni kwa hekima gani kuwaumba hawa, pamoja na kuwa mambo yao yatakuwa ni kuleta uharibifu katika ardhi na kumwaga damu kwa dhulma na uonevu, na hali sisi tuko chini ya amri yako: tunakutakasa na mabaya utakaso unaonasibiana na Sifa zako njema na utukufu Wako, na tunakusifu kwa kila sifa za ukamilifu na utukufu?” Allah Mtukufu Akasema kuwaambia, “Mimi najua msiyoyajua kuhusu uzito wa maslahi katika kuwaumba wao.”
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net