Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 29

Al-Baqara 2:29

البقرة

هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ لَكُم مَّا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ ٱسْتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ فَسَوَّىٰهُنَّ سَبْعَ سَمَـٰوَٰتٍ ۚ وَهُوَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ

Maana

Yeye ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyo katika ardhi, kisha akaelekea kuziumba mbingu, na akazifanya kuwa mbingu saba, naye ndiye ajuaye mno kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye aliye kuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi. Tena akazielekea mbingu, na akazifanya mbingu saba. Naye ndiye Mjuzi wa kila kitu. [29]

[29] Mwenyezi Mungu anaye pasa kuabudiwa na kut'iiwa ndiye aliye kufadhilini. Akaumba kwa ajili ya manufaa na faida yenu kila neema inayo patikana duniani, kisha baadae akazielekea mbingu akaziumba mbingu saba kwa mpango. Katika hayo yapo mnayo yaona na msiyo yaona. Na Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote, na anavijua vyote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu, Peke Yake, Ndiye Aliyeumba kwa ajili yenu kila kilichoko kwenye ardhi miongoni mwa neema ambazo mnanufaika nazo, kisha Akaelekea na kukusudia kuumba mbingu, Akazifanya mbingu saba. Na Yeye ni Mjuzi wa kila kitu, na elimu Yake, Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu, imevizunguka vitu vyote Alivyoviumba.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net