Al-Baqara 2:285
البقرةءَامَنَ ٱلرَّسُولُ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِ مِن رَّبِّهِۦ وَٱلْمُؤْمِنُونَ ۚ كُلٌّ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَمَلَـٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّن رُّسُلِهِۦ ۚ وَقَالُوا۟ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۖ غُفْرَانَكَ رَبَّنَا وَإِلَيْكَ ٱلْمَصِيرُ
Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake Mlezi, na Waumini vile vile. Wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutofautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumetii. Tunakutaka maghfira Mola wetu Mlezi! Na marejeo ni kwako.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mtume ameamini yaliyo teremshwa kwake kutoka kwa Mola Mlezi wake, na Waumini vile vile. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake na Mitume wake. Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake, na (Waumini) husema: Tumesikia na tumet'ii. Tunakutaka maghfira Mola Mlezi wetu! Na marejeo ni kwako. [285]
[285] Hakika aliyo teremshiwa Mtume Muhammad s.a.w. ni Haki itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Naye amemuamini Mwenyezi Mungu, na pamoja naye wameamini pia Waumini, wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake. Wao wanawaamini Mitume wote wa Mwenyezi Mungu sawa sawa, na wanawatukuza sawa, huku wakisema: Hatutafautishi baina ya yeyote katika Mitume wake. Na wametilia mkazo Imani yao ya moyoni kwa kauli yao ya ulimini huku wakimuelekea Mwenyezi Mungu kumwambia: Mola Mlezi wetu! Tumesikia uliyo yateremsha yenye hikima, na tumeyapokea yaliyo amrishwa. Ewe Mola wetu Mlezi! Tupe maghfira yako. Na kwako Wewe tu pekee ndio tunako kwendea na ndio marejeo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ameamini na kuyakinisha Mtume wa Allah Mtukufu, Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, yale aliyoletewa kwa njia ya wahyi kutoka kwa Mola wake. Na ni haki kwake aiyakinishe. Na Waumini pia wameamini na kufanya amali zinazoambatana na Qur’ani Tukufu. Kila mmoja katika wao amemuamini Allah Mtukufu kuwa ni Mola na Muabudiwa, Aliyesifika kwa sifa za utukufu na ukamilifu, na kuwa Allah Mtukufu Anao Malaika watukufu, na kuwa Yeye Ameteremsha Vitabu na Ametuma Mitume kwa waja Wake. Hatuwaamini, sisi Waumini, baadhi yao na kuwakanusha baadhi yao. Bali tunawaamini wao wote. Na wanasema, Mtume na Waumini, «Tumeusikia, ewe Mola wetu, wahyi uliouleta na tumetii katika yote hayo. Tunatarajia uyasamehe, kwa wema Wako, madhambi yetu. Wewe Ndiye Ambaye Uliyetulea kwa neema Zako Ulizotuneemesha nazo. Kwako Peke Yako ndio marejeo yetu na mwisho wetu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net