Al-Baqara 2:286
البقرةلَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۚ لَهَا مَا كَسَبَتْ وَعَلَيْهَا مَا ٱكْتَسَبَتْ ۗ رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَآ إِن نَّسِينَآ أَوْ أَخْطَأْنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تَحْمِلْ عَلَيْنَآ إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِنَا ۚ رَبَّنَا وَلَا تُحَمِّلْنَا مَا لَا طَاقَةَ لَنَا بِهِۦ ۖ وَٱعْفُ عَنَّا وَٱغْفِرْ لَنَا وَٱرْحَمْنَآ ۚ أَنتَ مَوْلَىٰنَا فَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَـٰفِرِينَ
Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kiwango cha iwezavyo. Faida ya iliyoyachuma ni yake, na hasara ya iliyoyachuma ni juu yake pia. (Semeni) Mola wetu Mlezi! Usituchukulie ubaya tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama uliyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi! Usitutwike tusiyoyaweza, na uyatupilie mbali mabaya yetu, na utusamehe na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi dhidi ya kaumu ya makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyho. Faida ya iliyo yachuma ni yake, na khasara ya iliyo yachuma ni juu yake pia. (Ombeni:)Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. [286]
[286] Hakika Mwenyezi Mungu hawakalifishi waja wake ila kwa kadiri wanavyo weza kuyafanya na kuyafuata. Kwa hivyo kila mwenye kukalifishwa atalipwa kwa vitendo vyake - akitenda kheri atapata malipo ya kheri, akitenda shari atapata shari. Basi enyi Waumini! Nyenyekeeni kwa Mwenyezi Mungu mkimuomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Usituadhibu pindi tukiporonyoka tukasahau ulio tuamrisha, au yakatupata ya kutusabibisha kutumbukia makosani. Mola Mlezi wetu! Usituchukulie kwa shida ukatupa sharia nzito nzito kama ulivyo wafanyia Mayahudi kwa sababu ya inda yao na udhalimu wao. Wala usitukalifishe mambo tusiyo yaweza, na utusamehe kwa ukarimu wako, na tughufirie kwa fadhila yako, na uturehemu kwa rehema yako yenye wasaa. Hakika Wewe ni Mola Mlezi wetu. Tunusuru ewe Mola Mlezi, kwa ajili ya kutukuza Neno lako na kuitangaza Dini yako - tuwashinde kaumu ya wapingaji.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Dini ya Allah Mtukufu ni sahali, haina uzito ndani yake. Allah Mtukufu hawatakii waja Wake wasiyoyaweza. Mwenye kufanya uzuri atapata uzuri, na mwenye kufanya ubaya atapata ubaya. Ewe Mola wetu! Usitutese tukisahau chochote miongoni mwa vitu ulivyotufaradhia au tukikosea kwa kufanya kitu chochote ulichotukataza kukifanya. Ewe Mola wetu! Na usitukalifishe kufanya matendo magumu uliyowakalifisha waliokuwa kabla yetu, miongoni mwa waasi, yakiwa ni mateso kwao. Ewe Mola wetu! Na usitubebeshe tusiyoyaweza ya amri ngumu na mikasa. Na uyafute madhambi yetu, uzisitiri aibu zetu na utufanyie wema. Wewe Ndiye Mwenye kuyamiliki mambo yetu na kuyaendesha. Tunusuru juu ya wale waliokataa Dini yako na kuukataa umoja wako na wakamkanusha Nabii wako Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, Na ujaalie mwisho mwema uwe ni wetu juu yao, Ulimwenguni na Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net