Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 284

Al-Baqara 2:284

البقرة

لِّلَّهِ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۗ وَإِن تُبْدُوا۟ مَا فِىٓ أَنفُسِكُمْ أَوْ تُخْفُوهُ يُحَاسِبْكُم بِهِ ٱللَّهُ ۖ فَيَغْفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ ۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi. Na mkidhihirisha yaliyo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu atawahesabu kwayo. Kisha atamsamehe amtakaye na amwadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Viliomo mbinguni na viliomo duniani ni vya Mwenyezi Mungu. Na mkidhihirisha yaliyomo katika nafsi zenu au mkayaficha, Mwenyezi Mungu atakuhisabuni kwayo. Kisha amsamehe amtakaye na amuadhibu amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. [284]

[284] Jueni kuwa vyote viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu, naye ana makdara navyo vyote na anavijua vyote. Ni sawa sawa ikiwa mtadhihirisha yaliyomo ndani ya nafsi zenu au mkificha, Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa vyote na mwenye kupata khabari za vyote. Naye Siku ya Kiyama atakuhisabuni kwa hayo, na atamghufiria amtakaye na atamuadhibu amtakaye. Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni wa Allah Mtukufu ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, kwa kuvimiliki, na kuvijua. Hakuna chochote kinachofichika Kwake. Na chochote mnachokidhihirisha, kati ya viliomo ndani ya nafsi zenu au mnachokificha, Allah Mtukufu Anakijua, na Atawahesabu nacho. Atamsamehe Anayemtaka na Atampatiliza Anayemtaka. Na Allah Mtukufu ni muweza wa kila kitu. Baadaye Allah Mtukufu aliwakirimu Waislamu Akasamehe maneno ya mtu kuiyambia nafsi yake na mawazo ya moyo, yakiwa hayatafuatiwa na maneno au vitendo, kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net