Al-Baqara 2:283
البقرةوَإِن كُنتُمْ عَلَىٰ سَفَرٍ وَلَمْ تَجِدُوا۟ كَاتِبًا فَرِهَـٰنٌ مَّقْبُوضَةٌ ۖ فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ ٱلَّذِى ٱؤْتُمِنَ أَمَـٰنَتَهُۥ وَلْيَتَّقِ ٱللَّهَ رَبَّهُۥ ۗ وَلَا تَكْتُمُوا۟ ٱلشَّهَـٰدَةَ ۚ وَمَن يَكْتُمْهَا فَإِنَّهُۥٓ ءَاثِمٌ قَلْبُهُۥ ۗ وَٱللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ
Na mkiwa katika safari, na hamkupata mwandishi, basi yatosha kukabidhiwa rahani. Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe, basi aliyeaminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala msifiche ushahidi. Na atakayeuficha, basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, yatosha kukabidhiwa rahani. Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe basi aliye aminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Mwenyezi Mungu, Mola wake Mlezi. Wala msifiche ushahidi. Na atakaye ficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mnayo yatenda. [283]
[283] Ikiwa mko safarini na hamkupata mtu wa kuliandika deni, basi kwa dhamana ya deni wekeni kitu kuwa ni rahani ashike mwenye kukopesha kutokana na mwenye kukopa. Na mtu akipewa dhamana na mwenzie kushika, basi iwe hiyo ni amana ilioko mikononi mwake. Yeye ametegemewa kwa uaminifu wake. Basi inapo takikana amana na aitoe amana ya watu. Na amche Mwenyezi Mungu aliye muumba na kumlea na kumshughulikia kwa uangalifu ili isimkatikie neema ya Mola wake Mlezi duniani na Akhera. Wala msifiche ushahidi unapo takikana. Mwenye kuficha amepata dhambi, na khabithi wa moyo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua mnayo yafanya. Atakulipeni kwa mujibu mnavyo stahiki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mkiwa muko safarini, na msipate mwenye kuwaandikia, mpatieni yule mwenye haki kitu kiwe ni dhamana ya haki yake hadi mdaiwa atakapolipa deni yake. Na iwapo nyinyi kwa nyinyi mumeaminiana, hapana makosa kuacha kuandika, kushuhudisha na kuweka rahani, na deni itabaki ni amana kwenye shingo ya mdaiwa, ni juu yake kuilipa. Na ni juu yake amche Allah Mtukufu asimfanyiye hiana mwenzake. Na akikataa mdaiwa deni iliyo juu yake, na ikawa pana mtu aliyekuweko na kushuhudia, huyo itamlazimu kuutoa wazi ushahidi wake. Na mwenye kuuficha ushahidi huu, ni mtu mwenye moyo wa hiana na urongo. Na Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kuona siri zote, Ndiye Ambaye ujuzi Wake umezunguka mambo yenu yote, na Atawahesabu kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net