Al-Baqara 2:278
البقرةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَذَرُوا۟ مَا بَقِىَ مِنَ ٱلرِّبَوٰٓا۟ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ
Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizobaki, ikiwa nyinyi ni Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni riba zilizo bakia, ikiwa nyinyi ni Waumini. [278]
[278] Enyi mlio amini! Mwogopeni Mwenyezi Mungu, na wacheni heba yake na khofu yake ijae katika nyoyo zenu, na wacheni kudai hiyo riba iliyo bakia juu ya shingo za watu ikiwa ni kweli nyinyi ni Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na mkamfuata Mtume Wake, muogopeni Allah Mtukufu na muache kutaka ziada iliyosalia juu ya rasilmali zenu, ambayo mlistahiki kupata kabla riba haijaharamishwa, iwapo imani yenu ni ya kidhati kimaneno na kivitendo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net