Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 279

Al-Baqara 2:279

البقرة

فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا۟ فَأْذَنُوا۟ بِحَرْبٍ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَٰلِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ

Maana

Na msipofanya, basi jitangazieni vita kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilimali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe. [279]

[279] Ikiwa hamfanyi aliyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu kuacha riba basi kuweni na yakini kuwa nyinyi mko vitani na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa sababu ya inadi yenu kuipinga amri ya Mwenyezi Mungu. Ikiwa mnataka toba ya kukubaliwa basi haki yenu ni kuchukua ile rasilmali yenu tu. Msichukue kitu zaidi, kidogo au kingi, bila ya kujali sababu ya hilo deni na vipi lilivyo tumiwa. Kwani hiyo ziada mnayo ichukua ni kumdhulumu mtu, kama vile kuacha sehemu ya rasilmali yenu ni dhulma juu yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Msipokomeka na hilo mlilokatazwa na Allah Mtukufu, basi kuweni na yakini ya vita kutoka kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake, na mkirudi kwa Mola wenu na mkaacha kula riba, ni haki yenu mchukue madeni yenu bila ya nyongeza, hamumdhulumu yoyote kwa kuchukua zaidi ya rasilmali zenu wala hamudhulumiwi na yoyote kwa kupunguza kiwango cha pesa mlichokopesha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net