Al-Baqara 2:277
البقرةإِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُا۟ ٱلزَّكَوٰةَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ وَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
Hakika, wale walioamini na wakatenda mema na wakashika Swala na wakatoa Zaka, wao watapata ujira wao kwa Mola wao Mlezi. Wala haitakuwa hofu juu yao, wala hawatahuzunika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wale walio amini na wakatenda mema na wakashika Swala na wakatoa Zaka, wao watapata ujira wao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa khofu juu yao, wala hawatahuzunika. [277]
[277] Hakika wale wanao muamini Mwenyezi Mungu, na wakazitimiza amri zake, na wakatenda mema aliyo waamrisha, na wakaacha yaliyo katazwa ya haramu, na wakatimiza Swala kwa njia ya ukamilifu, na wakatoa Zaka kuwapa wanao stahiki, watapata thawabu kubwa mno walio wekewa kwa Mola wao. Na wala hawatakuwa na khofu ya chochote kwa siku zijazo, wala hawatahuzunika kwa lolote walilo likosa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakatenda matendo mema, wakatekeleza Swala kama Alivyoamrisha Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakatoa Zaka za mali yao, wana thawabu kubwa zinazowahusu wao mbele ya Mola wao na Mruzuku wao. Na hawatapatwa na woga katika Akhera yao, wala masikitiko juu ya mambo mazuri ya kilimwengu waliyoyakosa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net