Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 276

Al-Baqara 2:276

البقرة

يَمْحَقُ ٱللَّهُ ٱلرِّبَوٰا۟ وَيُرْبِى ٱلصَّدَقَـٰتِ ۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ

Maana

Mwenyezi Mungu huondoa baraka katika riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukufuru mno na afanyae dhambi nyingi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi. [276]

[276] Mwenyezi Mungu huondoa ile ziada iliyo twaliwa kuwa ni riba juu ya mali yaliyo kopeshwa, na huitilia baraka mali iliyo tolewa sadaka, na huilipia thawabu mara nyingi kuliko kile kilicho tolewa. Na Mwenyezi Mungu hawapendi watu wanao endelea kuhalalisha haramu kama riba, wala wale wanao endelea kuchukua riba.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anaiyondoa riba yote au Anamnyima mlaji riba baraka ya mali yake asinufaike nayo. Na Anazikuza sadaka na kuzifanya ziwe nyingi na Anawaongezea malipo wenye kutoa sadaka maradufu na Anawabarikia katika mali yao. Na Allah Mtukufu Hampendi kila mwenye kushikilia kwenye ukafiri wake, mwenye kujihalalishia ulaji riba, mwenye kukolea ndani ya dhambi na haramu na kumuasi Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net