Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 27

Al-Baqara 2:27

البقرة

ٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مِيثَـٰقِهِۦ وَيَقْطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ

Maana

Wale wanaovunja agano la Mwenyezi Mungu baada ya kwishalifunga, na wakayakata aliyoamrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika ardhi; hao ndio wenye hasara.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kwisha ifunga, na wakayakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu kuungwa, na wakafanya uharibifu katika nchi; hao ndio wenye khasara. [27]

[27] Na hao walio kwisha potea ni wale ambao wanaivunja ahadi ya Mwenyezi Mungu, na wao ndio wasio ishika vilivyo ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyo iweka katika nafsi zao tangu kuumbwa, kuwa ni fungamano la akili yenye kutambua na yenye kuunga mkono Utume, na wakayakata yale aliyo yaamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, kama vile kuwaangalia jamaa, na kupendana na kutendeana mema, na kuoneana hurumu watu kwa watu; na wakafanya fisadi katika nchi kwa mambo maovu na kuzua fitna na kuchochea vita na kuharibu majenzi. Hao ndio wenye kuleta khasara kwa kufisidi khulka yao walio umbwa nayo, na wakawagawa watu mapande mapande, badala ya kuleta mapenzi na kuoneana huruma kama inavyo stahiki. Kwa vitendo vyao hivyo watapata hizaya duniani na adhabu huko Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale ambao wanavunja ahadi ya Allah Mtukufu Aliyoichukuwa kwao kuwa wampwekeshe Yeye na wamtii, hali ya kuwa Ameitilia mkazo ahadi hiyo kwa kuleta Mitume na kuteremsha vitabu, na wanaenda kinyume na dini ya Allah Mtukufu, kama kukata zao na kueneza uharibifu katika ardhi. Basi wao ndio wenye hasara duniani na Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net