Al-Baqara 2:258
البقرةأَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِى حَآجَّ إِبْرَٰهِـۧمَ فِى رَبِّهِۦٓ أَنْ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلْمُلْكَ إِذْ قَالَ إِبْرَٰهِـۧمُ رَبِّىَ ٱلَّذِى يُحْىِۦ وَيُمِيتُ قَالَ أَنَا۠ أُحْىِۦ وَأُمِيتُ ۖ قَالَ إِبْرَٰهِـۧمُ فَإِنَّ ٱللَّهَ يَأْتِى بِٱلشَّمْسِ مِنَ ٱلْمَشْرِقِ فَأْتِ بِهَا مِنَ ٱلْمَغْرِبِ فَبُهِتَ ٱلَّذِى كَفَرَ ۗ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Kwani hukumuona yule aliyehojiana na Ibrahim kuhusu Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim aliposema: Mola wangu Mlezi ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia ninahuisha na ninafisha. Ibrahim akasema: Kwa hakika, Mwenyezi Mungu hulileta jua kutokea mashariki, basi wewe lilete kutokea magharibi. Kwa hivyo, akashindwa yule aliyekufuru. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu dhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hukumwona yule aliye hojiana na Ibrahim juu ya Mola wake Mlezi kwa sababu Mwenyezi Mungu alimpa ufalme? Ibrahim alipo sema: Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha. Yeye akasema: Mimi pia nahuisha na kufisha. Ibrahim akasema: Mwenyezi Mungu hulichomozesha jua mashariki, basi wewe lichomozeshe magharibi. Akafedheheka yule aliye kufuru; na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu. [258]
[258] Humwoni yule aliye pofuka asizione dalili za Imani akajadiliana na Ibrahim, rafiki wa Mwenyezi Mungu, katika uungu wa Mola wake Mlezi na Umoja wake, na vipi alivyo danganyika na ufalme wake alio pewa na Mola wake Mlezi hata akatoka kwenye nuru ya maumbile akaingia katika kiza cha ukafiri? Alipo sema Ibrahim: Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha, kwa kuitia roho katika kiwiliwili na kuitoa, yule mfalme kafiri akasema: Nami nahuisha na ninafisha kwa kusamehe na kuuwa. Basi Ibrahim akamwambia ili kuyakata majadiliano: Mwenyezi Mungu analichomozesha jua mashariki, basi wewe lileta litoke magharibi kama wewe ni mungu kama unavyo dai. Akahizika, na majadiliano yakakatika kwa nguvu za hoja zilizo kashifu udhaifu wake na kughurika kwake. Na Mwenyezi Mungu hawawezeshi wakaidi na wenye inadi kufuata Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je umewahi kuona, ewe Mtume, hali ya kustaajabisha zaidi kuliko ile ya yule aliyemjadili Ibrãhîm, amani imshukie, juu ya kumpwekesha Allah Mtukufu na juu ya umola Wake, kwa kuwa Allah Mtukufu Alimpa ufalme, alipofanya ujeuri na kumuuliza Ibrãhîm, «Ni nani Mola wako?» Alisema, amani imshukie, «Mola wangu ni Ambaye Anavipa viumbe uhai vikahuika na Anaviondolea uhai vikafa. Yeye Ndiye Aliyepwekeka kwa kuhuisha na kufisha.» Akasema, «Mimi nahuisha na kufisha.» Yaani: namuua nimtakaye kumuua, na namuachilia nimtakaye kumuachilia. Ibrãhîm akasema kumwambia, «Allah Mtukufu ninayemuabudu Analitoa jua upande wa mashariki. Je unaweza wewe kugeuza mwenendo huu wa kimungu, ulifanye litokeze upande wa magharibi?» Akapigwa na mshangao huyu kafiri na ikakatika hoja yake. Hali yake ni ile ya madhalimu, Allah Mtukufu Hawaongozi kwenye haki na usawa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net