Al-Baqara 2:257
البقرةٱللَّهُ وَلِىُّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يُخْرِجُهُم مِّنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ ۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَوْلِيَآؤُهُمُ ٱلطَّـٰغُوتُ يُخْرِجُونَهُم مِّنَ ٱلنُّورِ إِلَى ٱلظُّلُمَـٰتِ ۗ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ
Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa walioamini. Huwatoa katika giza mbalimbali kwenda katika nuru. Lakini wale waliokufuru, walinzi wao ni Taaghut. Huwatoa katika nuru kwenda hadi katika giza mbalimbali. Hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Huwatoa gizani na kuwaingiza mwangazani. Lakini walio kufuru, walinzi wao ni Mashet'ani. Huwatoa kwenye mwangaza na kuwaingiza gizani. Hao ndio watu wa Motoni, na humo watadumu. [257]
[257] Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuyaangalia mambo ya Waumini, na ndiye Mwenye kuwasaidia na kuwanusuru. Huwatoa kwenye kiza cha shaka na kudanganyikiwa kuendea kwenye nuru ya Haki na utulivu. Na Makafiri wenye kumkanya Mwenyezi Mungu wanashughulikiwa na Mashetani na wanao lingania shari na upotovu. Wao hao huwatoa kwenye nuru ya Imani walio umbiwa nayo na iliyo zagaa kwa dalili nyingi na ishara, na kuwatia kwenye kiza cha ukafiri na ufisadi. Na hawa makafiri ndio watu wa Motoni, na humo watadumu milele.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Anawasimamia Waumini kwa kuwanusuru, kuwaafikia na kuwahifadhi, Anawatoa kutoka kwenye magiza ya ukafiri kuwapeleka kwenye nuru ya Imani. Na wale waliokufuru, wanusuru wao na wasaidizi wao ni wale wafananishwao na Allah Mtukufu na masanamu wanaowaabudu wasiokuwa Allah Mtukufu. Hao wanawatoa wao kutoka kwenye nuru ya Imani kuwapeleka kwenye magiza ya ukafiri. Wao ndio watu wa Motoni, wenye kusalia humo milele na si wenye kutoka humo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net