Al-Baqara 2:256
البقرةلَآ إِكْرَاهَ فِى ٱلدِّينِ ۖ قَد تَّبَيَّنَ ٱلرُّشْدُ مِنَ ٱلْغَىِّ ۚ فَمَن يَكْفُرْ بِٱلطَّـٰغُوتِ وَيُؤْمِنۢ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱسْتَمْسَكَ بِٱلْعُرْوَةِ ٱلْوُثْقَىٰ لَا ٱنفِصَامَ لَهَا ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Hakuna kulazimisha katika Dini. Kwani uongofu umekwishapambanuka kutokana na upotovu. Kwa hivyo, anayemkufuru Taaghuut na akamwamini Mwenyezi Mungu, basi bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisichovunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia mno, Mwenye kujua vyema.[1]
[1] Na wala hakuna upinzani baina ya maana hii na Aya nyingi zinazolazimu kuwepo kwa Jihadi. Kwani, Mwenyezi Mungu ameamrisha kupigana vita ili Dini yote iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kuzuia uadui wa wenye kufanya uadui dhidi ya dini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua. [256]
[256] Hapana ruhusa kumlazimisha yeyote kuingia katika Dini. Kwa Aya na Ishara zilio zagaa Njia ya Haki imewekwa wazi kutokana na njia ya upotovu. Basi aliye ongoka akafuata Imani na akakataa kufuata chochote kisicho ingia akilini, na kinacho mpelekea kuacha Haki, basi huyo ameshika njia madhbuti kabisa ya kumkinga asiingie katika upotovu, kama yule mwenye kukamata kishikio imara kilicho fungika baraabara kitacho mlinda asitumbukie shimoni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyasikia mnayo yasema, ni Mwenye kuyajua mnayo yatenda, na ni Mwenye kukulipeni kwa vitendo vyenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa kuwa Dini hii imekamilika na hoja zake ziko wazi, haihitajii ilazimishwe kwa watu ambao jizya (jizyah) inapokewa kutoka kwao. Kwani dalili ziko wazi ambazo kwa dalili hizo inabainika haki, ikawa kando na batili, na uongofu, ukawa kando na upotevu. Basi mwenye kukanusha vyote vinavyoabudiwa badala ya Allah Mtukufu na akamuamini Allah Mtukufu, huwa amethibiti na kulingana kwenye njia bora na ameshikamana na kamba imara ya Dini isiyokatika. Na Allah Mtukufu ni Msikizi wa maneno ya waja Wake, ni Mjuzi wa nia zao na vitendo vyao na Atawalipa kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net