Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 252

Al-Baqara 2:252

البقرة

تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱللَّهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِٱلْحَقِّ ۚ وَإِنَّكَ لَمِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ

Maana

Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunazokusomea kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hizi ni Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki. Na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume. [252]

[252] Kisa hichi ni katika mafunzo ya kuzingatia tunakusimulia kwa kweli, ili kiwe ni ruwaza kwako na dalili ya ukweli wa Utume wako, na ili ujue kuwa Sisi hakika tutakunusuru kama tulivyo wanusuru Mitume walio kuwa kabla yako.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hizo ni hoja za Allah Mtukufu na dalili Zake tunakusimulia wewe kwa haki, ewe Nabii, na hakika wewe ni miongoni mwa Mitume walio wakweli.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net