Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 251

Al-Baqara 2:251

البقرة

فَهَزَمُوهُم بِإِذْنِ ٱللَّهِ وَقَتَلَ دَاوُۥدُ جَالُوتَ وَءَاتَىٰهُ ٱللَّهُ ٱلْمُلْكَ وَٱلْحِكْمَةَ وَعَلَّمَهُۥ مِمَّا يَشَآءُ ۗ وَلَوْلَا دَفْعُ ٱللَّهِ ٱلنَّاسَ بَعْضَهُم بِبَعْضٍ لَّفَسَدَتِ ٱلْأَرْضُ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ ذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Kwa hivyo, wakawashinda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na Daudi akamuua Jaluti. Na Mwenyezi Mungu akampa Daudi ufalme na hekima, na akamfundisha katika aliyoyataka. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawazuii watu kwa watu, basi dunia ingeliharibika. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu wote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

--Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu waliwatimua, na Daudi akamuuwa Jaluti, na Mwenyezi Mungu akampa Daudi ufalme na hikima, na akamfundisha aliyo yapenda. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawapambanishi watu kwa watu basi dunia ingeli haribika. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya walimwengu wote. [251]

[251] Basi wale Waumini waliwashinda maadui zao kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Daudi, mmoja wa askari wa Taluti, akamwuuwa Jaluti amiri-jeshi wa makafiri. Na Mwenyezi Mungu akampa Daudi utawala baada ya Twaluti. Akampa na unabii na ilimu yenye manufaa, na akamfunza kwa ayapendayo Mwenyezi Mungu. Na huo ndio mwendo wake Mwenyezi Mungu - kuwanusuru wale wanao tenda mema duniani wala hawafanyi ufisadi. Lau kuwa Mwenyezi Mungu hawasalitishi askari wake kupambana na mafisadi kwa ajili ya kuondoa ufisadi wao, na akawasalitisha waovu wenyewe kwa wenyewe, ulimwengu usingeli endelea. Lakini Mwenyezi Mungu ni Mwenye hisani na fadhila daima milele juu ya waja wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapo waliwashinda kwa idhini ya Allah Mtukufu, na Dāwūd, Amani imshukiye, alimuua Jālūt, kiongozi wa majabari. Na Allah Mtukufu, Aliyeshinda na kutukuka, baada ya hapo, Akampa Dāwūd ufalme na utume katika Wana wa Isrãîl, na Alimfundisha Aliyoyataka miongoni mwa elimu. Na lau kama si himaya ya Allah Mtukufu, kwa kuwatumia baadhi ya watu- nao ni wale watiifu Kwake na wanaomuamini- kuwazuia wengine- nao ni wanaomuasi Allah Mtukufu na kumshirikisha-, basi ardhi ingaliharibika kwa ushindi wa ukafiri na kupata nguvu uharibifu na wenye kufanya maasia. Lakini Allah Mtukufu ni Mwenye fadhila kwa viumbe wote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net