Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 250

Al-Baqara 2:250

البقرة

وَلَمَّا بَرَزُوا۟ لِجَالُوتَ وَجُنُودِهِۦ قَالُوا۟ رَبَّنَآ أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَٱنصُرْنَا عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Na walipotoka ili kupambana na Jaluti na majeshi yake, walisema: Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utunusuru kutokana na watu hawa makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na walipo toka kupambana na Jaluti na majeshi yake walisema: Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri. [250]

[250] Waumini walipo songa kupigana na Jaluti na jeshi lake walimwelekea Mwenyezi Mungu wakamnyenyekea na kumwomba awajaze subira, awatie nguvu azma zao, naawaweke imara katika uwanja wa vita, na awape ushindi juu ya maadui zao makafiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na walipojitokeza kwa Jālūt na askari wake na wakaiona hatari kwa macho yao, walifazaika na kumuelekea Allah Mtukufu kwa maombi na kunyenyekea huku wakisema, Ewe Mola wetu! Tumiminie subira nyingi kwenye nyoyo zetu, Uzithibitishe nyayo zetu ziwe thabiti muda wa kupigana na adui, zisiwe na uoga wa kukimbia vita, na Utunusuru kwa msaada wako juu ya watu makafiri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net