Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 248

Al-Baqara 2:248

البقرة

وَقَالَ لَهُمْ نَبِيُّهُمْ إِنَّ ءَايَةَ مُلْكِهِۦٓ أَن يَأْتِيَكُمُ ٱلتَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَبَقِيَّةٌ مِّمَّا تَرَكَ ءَالُ مُوسَىٰ وَءَالُ هَـٰرُونَ تَحْمِلُهُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Maana

Na Nabii wao akawaambia: Hakika, alama ya ufalme wake ni kwamba awaletee lile sanduku ambalo ndani yake mna kituliza nyoyo zenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na mabaki ya waliyoyaacha watu wa Musa na watu wa Harun, linalobebwa na Malaika. Bila shaka, katika hayo zimo ishara kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Nabii wao akawaambia: Alama ya ufalme wake ni kukuleteeni lile sanduku ambalo mna ndani yake kituliza nyoyo zenu, kitokacho kwa Mola wenu Mlezi, na mna mabaki ya waliyo yaacha kina Musa na kina Harun, wanalichukua Malaika. Bila shaka katika hayo zimo dalili kwenu ikiwa nyinyi mnaamini. [248]

[248] Na Nabii wao aliwaambia: "Hakika dalili ya ukweli wangu kuwa Mwenyezi Mungu amemteua Twaluti awe ni mtawala wenu ni kuwa atakurejesheeni sanduku la Taurati mlio nyang'anywa, linalo bebwa na Malaika. Na ndani yake yamo baadhi ya mabaki ya watu wa Musa na watu wa Harun walio kuja baada yao. Na likiletwa sanduku hilo nyoyo zenu zitatua. Katika hayo hakika pana dalili ambazo zitakupelekeeni kumfuata na kumridhia, ikiwa kama kweli nyinyi mnataka Haki na mnaiamini."

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mtume wao aliwaambia, «Hakika alama ya ufalme wake ni kuwajilieni sanduku ambalo ndani yake muna Taurati.- Sanduku ambalo maadui wao walikuwa wamewanyang’anya-. Ndani yake muna utulivu kutoka kwa Mola wenu unaozithibitisha nyoyo za wenye ikhlasi. Na muna ndani yake mabaki ya vitu vilivyoachwa na jamaa za Mûsã na jamaa za Harun, kama fimbo na vipande vya mbao, yanabebwa na Malaika. Hakika muna katika hayo hoja kubwa kuwa Ṭālūt amechaguliwa kuwa mfalme wenu kwa amri ya Allah Mtukufu, iwapo mnamuamini Allah Mtukufu na Mitume Wake».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net