Al-Baqara 2:24
البقرةفَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا۟ وَلَن تَفْعَلُوا۟ فَٱتَّقُوا۟ ٱلنَّارَ ٱلَّتِى وَقُودُهَا ٱلنَّاسُ وَٱلْحِجَارَةُ ۖ أُعِدَّتْ لِلْكَـٰفِرِينَ
Na ikiwa hamtafanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mkitofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe walio andaliwa hao wanao kanusha. [24]
[24] Basi ikiwa hamtoweza kuleta sura moja mfano wa hizi sura za Qur'ani - na kabisa hamtoweza kwa njia yoyote, kwani viumbe hawawezi hayo kwa kuwa Qura'ani ni maneno ya Muumba - basi waajibu wenu mziepuke sababu zitazo kuleteeni adhabu ya akhera, nayo ni Moto ambao utakuwa kuni zake za kuwashia ni hao makafiri na masanamu yao. Moto huu umetengenezwa kwa ajili ya kuwaadhibu wapinzani wenye inda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mkiwa hamuwezi sasa, na hamtaweza wakati unaokuja kabisa, basi uogopeni Moto, kwa kumuamini Nabii, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na kumtii Allah Mtukufu. Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, umeandaliwa wenye kumkanusha Allah Mtukufu na Mitume Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net