Al-Baqara 2:23
البقرةوَإِن كُنتُمْ فِى رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا فَأْتُوا۟ بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِۦ وَٱدْعُوا۟ شُهَدَآءَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyomteremshia mja wetu, basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu kando na Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja wetu basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli. [23]
[23] Na ikiwa mna shaka kuisadiki hii Qur'ani tunayo mteremshia mja wetu Muhammad, basi mnayo hoja iliyo dhaahiri itayo kubainishieni haki: jaribuni kuleta sura kama hizi za Qur'ani katika ufasihi wake, na hukumu zake, na ilimu zake, na uwongofu wake wote, na muwaite watakao shuhudia kwamba mmeleta sura mfano wake, mtake msaada kwao, na wala hamtowapata. Na mashahidi hao ni mbali na Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu anamuunga mkono mja wake kwa hichi Kitabu chake, na anamshuhudia kwa vitendo vyake. Haya ikiwa ni kweli nyinyi mnaitilia shaka hii Qur'ani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mkiwa, enyi makafiri, muna shaka juu ya Qur,ani tuliyomteremshia mja wetu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani imshukie, na mkadai kuwa haitoki kwa Allah Mtukufu, basi leteni sura moja inayofanana na sura ya Qurani, na takeni msaada kutoka kwa yoyote mnayemuweza ili awasaidie, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net