Al-Baqara 2:232
البقرةوَإِذَا طَلَّقْتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَبَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَلَا تَعْضُلُوهُنَّ أَن يَنكِحْنَ أَزْوَٰجَهُنَّ إِذَا تَرَٰضَوْا۟ بَيْنَهُم بِٱلْمَعْرُوفِ ۗ ذَٰلِكَ يُوعَظُ بِهِۦ مَن كَانَ مِنكُمْ يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ ۗ ذَٰلِكُمْ أَزْكَىٰ لَكُمْ وَأَطْهَرُ ۗ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
Na mtakapowataliki wanawake, nao wakamaliza muda wao (wa eda), basi msiwazuie kuoleka kwa waume zao endapo baina yao wamekubaliana kwa wema. Hayo anawaidhiwa kwayo yule miongoni mwenu anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ni bora zaidi kwenu na safi kabisa. Na Mwenyezi Mungu anajua, lakini nyinyi hamjui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mtakapo wapa wanawake t'alaka nao wakamaliza eda yao, basi msiwazuie kuolewa na waume zao endapo baina yao wamepatana kwa wema. Hayo anaonywa nayo yule miongoni mwenu anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ni bora zaidi kwenu na safi kabisa. Na Mwenyezi Mungu anajua, lakini nyinyi hamjui. [232]
[232] Mmnapo waacha wake na zikatimia eda na akitaka mwanamke kuanza maisha mapya kwa kuolewa tena ama na yule mku-mwenziwe au na mwanamume mwengine, basi si halali kwa wazee wala yule mku-mwenza kuwakataza, ikiwa pande mbili zimeridhiana kufanya ndoa mpya kwa kutaka maisha bora yatakayo pelekea masikilizano mema baina yao. Anawaidhiwa hayo anaye muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Mwendo huo unapelekea kukuza mahusiano ya hishima na sharaf katika jamii zenu, na ni usafi zaidi katika nafsi zenu kut'ahirika na uchafu na mahusiano yaliyo maovu. Na Mwenyezi Mungu anajua maslaha ya binaadamu na siri za nafsi zao ambazo wao hawajui vipi kuzipata.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na mtakapowaacha wake zenu chini ya talaka tatu na eda lao likaisha bila nyinyi kuwarejea, basi msiwadhiki, enyi mawalii, hao walioachwa kwa kuwazuia kurudi kwa waume zao, kwa kufunga ndoa upya, wakiwa wenyewe wametaka hilo na yakapatikana maridhiano kisheria na kidesturi. Hilo aidhiwa kwalo Aliyekuwa miongoni mwenu ni mkweli kwenye imani yake kwa Allah Mtukufu na Siku ya Mwisho. Hakika kuacha kuwazuia na kuwawezesha waume kuwaoa waliokuwa wake zao, ni jambo lenye kukuza zaidi na kutakasa zaidi heshima zenu, na ni lenye nafuu kubwa zaidi na thawabu nyingi zaidi kwenu. Na Allah Mtukufu Anayajua yenye maslahi kwenu; na nyinyi hamjui hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net