Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 230

Al-Baqara 2:230

البقرة

فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُۥ مِنۢ بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُۥ ۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَآ أَن يَتَرَاجَعَآ إِن ظَنَّآ أَن يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ ٱللَّهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ

Maana

Na akimtaliki (talaka ya tatu), basi yeye si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume asiyekuwa yeye. Na (huyo mwingine) akimtaliki, basi hakuna ubaya kwao (mke na mume wa kwanza) kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayoibainisha kwa watu wanaojua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kama amempa t'alaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwengine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayo ibainisha kwa watu wanao jua. [230]

[230] Mume akimwacha mkewe mara ya tatu baada ya T'alaka mbili za mwanzo basi hamhalalikii mpaka yule mke aolewe na mume mwengine aingie harusi. Akimwacha baada ya hapo basi anaweza kufunga ndoa tena na yule mume wa kwanza, na wala hapana dhambi juu yao kuanza maisha mapya kwa ndoa mpya. Lakini yawapasa waazimie kuendesha maisha mema ya mume na mke wakifuata sharia alizo ziwekea mipaka Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la. Na mipaka hii imebainishwa wazi kwa mwenye kuamini sharia ya Kiislamu na anataka ilimu na a'mali njema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iwapo mume atamtaliki mkewe talaka ya tatu, basi mke huyo atakuwa si halali tena kwa mume huyo, isipokuwa atakapoolewa na mwanamume mwengine ndoa sahihi na akaingiliwa katika ndoa hiyo, iwapo ndoa hiyo ni ya kutakana, na si kwa nia ya kumhalalisha yule mwanamke kwa mume wake wa kwanza. Na iwapo yule mume mwengine atamuacha mke yule, au akafa na eda lake likaisha, basi hapana dhambi kwa yule mwanamke na mume wake wa kwanza kuoana kwa kifungo cha ndoa kipya na mahari mapya, ikiwa wawili hao waonelea kwamba watazitekeleza hukumu za Allah Mtukufu Alizoziweka kwa waliooana. Hizo ni sheria za Allah Mtukufu zilizowekewa mipaka, Anazifunua wazi kwa watu wanaozijua hukumu Zake na mipaka Yake, kwani ni wao wanaonufaika nazo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net