Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 226

Al-Baqara 2:226

البقرة

لِّلَّذِينَ يُؤْلُونَ مِن نِّسَآئِهِمْ تَرَبُّصُ أَرْبَعَةِ أَشْهُرٍ ۖ فَإِن فَآءُو فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Kwa wale wanaoapa kujitenga na wake zao, wangojee miezi minne. Na wakirejea, basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kwa wanao apa kuwa watajitenga na wake zao, wangojee miezi mine. Wakirejea basi Mwenyezi Mungu hakika ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. [226]

[226] Na hawa walio apa kuwa hawatawakaribia wake zao, na wangoje muda wa miezi mine. Wakiwaingilia wake zao mnamo muda huu ndoa itaendelea, lakini juu yao ni kafara kwa yamini yao. Na Mwenyezi Mungu amewasamehe na anakubali kafara kwa rehema yake kuwahurumia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale wanaoapa kwa Allah Mtukufu kwamba hawatawaingilia wake zao, wana muda wa kusubiriwa wa miezi min` ne. Iwapo watarudi kabla kumalizika hiyo miezi mine, basi Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasamehe makosa yaliyofanywa na wao ya kiapo kwa sababu ya kurudi kwao, ni Mwenye huruma nao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net