Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 225

Al-Baqara 2:225

البقرة

لَّا يُؤَاخِذُكُمُ ٱللَّهُ بِٱللَّغْوِ فِىٓ أَيْمَـٰنِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا كَسَبَتْ قُلُوبُكُمْ ۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٌ

Maana

Mwenyezi Mungu hawachukulii ubaya katika viapo vyenu ambavyo hamkuvikusudia. Lakini anawachukulia ubaya kwa yale ambayo nyoyo zenu zinachuma. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mpole.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu hakushikeni kwa viapo vyenu vya upuuzi. Bali anakushikeni kwa yanayo chuma nyoyo zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mpole. [225]

[225] Mwenyezi Mungu amekusameheni baadhi ya yamini (viapo) zenu. Lilio mpitia mtu ulimini mwake katika viapo bila ya kukusudia wala kulitia moyoni, au akaapa kwa kuamini kuwa limetukia na halikutukia, Mwenyezi Mungu hayachukulii hayo. Lakini anakushikeni kwa mnayo yaazimia katika nyoyo zenu kuwa yamekuwa au hayakuwa, na kwa kusema uwongo pamoja na kuuwapia yamini. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kumghufiria mwenye kutubu, ni Mpole, anasamehe lisilo kusudiwa moyoni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Hatawaadhibu nyinyi kwa sababu ya viapo vyenu mnavyoviapa bila kukusudia, lakini Atawaadhibu kwa viapo vilivyokusudiwa na nyoyo zenu. Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe kwa yule anayetubia Kwake, ni Mpole kwa mwenye kumuasi kwa kuwa hamharakishii mateso.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net