Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 224

Al-Baqara 2:224

البقرة

وَلَا تَجْعَلُوا۟ ٱللَّهَ عُرْضَةً لِّأَيْمَـٰنِكُمْ أَن تَبَرُّوا۟ وَتَتَّقُوا۟ وَتُصْلِحُوا۟ بَيْنَ ٱلنَّاسِ ۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Maana

Wala msifanye Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu kuwa kisingizio cha kuacha kufanya wema, na kumcha Mungu, na kupatanisha baina ya watu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wala msifanye jina la Mwenyezi Mungu katika viapo vyenu kuwa ni kisingizio cha kuacha kufanya wema na kuchamngu na kupatanisha baina ya watu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kujua. [224]

[224] Msilichezee jina la Mwenyezi Mungu katika kukithirisha viapo, kwani hivyo inakuwa ni kinyume na kulitukuza jina la Mwenyezi Mungu. Na hakika kujilinda na kukithirisha kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ndio hupelekea vitendo vyema, na kuchamngu, na kuweza kusuluhisha baina ya watu. Mwenye kujilinda hivyo huwa anatukuka cheo katika macho ya watu, na anakuwa anaaminika, na kauli yake hukubalika kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia maneno yenu na yamini zenu, na Mjuzi wa niya zenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wala msikifanye, enyi Waislamu, kiapo chenu kwa Allah Mtukufu kuwa ni chenye kuwazuia nyinyi kufanya wema, kuunga kizazi, kumcha Allah Mtukufu na kusuluhisha kati ya watu. Nako ni iwapo mtaitwa kufanya lolote katika hayo, mkakataa na kutoa hoja kwamba mliapa kwa Allah Mtukufu kuwa hamtalifanya. Bali ni juu ya Mwenye kuapa ageuze kiapo chake, afanye vitendo vya kheri na atoe kafara ya kiapo chake wala asizowee jambo hilo. Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasikia maneno yenu, ni Mwenye kuzijua hali zenu zote.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net