Al-Baqara 2:223
البقرةنِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُوا۟ حَرْثَكُمْ أَنَّىٰ شِئْتُمْ ۖ وَقَدِّمُوا۟ لِأَنفُسِكُمْ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُم مُّلَـٰقُوهُ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Wake zenu ni konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini zitangulizieni heri nafsi zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana naye. Na wape habari njema Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo. Lakini jitangulizieni kheri nafsi zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu, na jueni kuwa hakika nyinyi mtakutana naye. Na wape bishara njema Waumini. [223]
[223] Wake zenu ni mwahali mwa kupatia uzazi, kama vile mbegu inavyo toa mmea. Basi ni halali kwenu kuwaingilia vyovyote kwa sharti ya kupitia njia za uzazi. Na mcheni Mwenyezi Mungu wala msimuasi katika kukaa kwenu na wanawake. Na mjue kuwa nyinyi mtakutana naye, na mna jukumu kwake. Furaha ni ya hao wanao simama juu ya mipaka yake Mtukufu na hawaikiuki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wake zenu ni pahali pa makulima yenu, mnaweka tone la manii ndani ya uzao wao, wakatoka humo watoto kwa matakwa ya Allah Mtukufu. Kwa hivyo, waingilieni pale pahali pake pa kuingiliwa tu, napo ni tupu ya mbele, kwa namna yoyote mtakayo. Na zitangulizieni nafsi zenu amali njema kwa kuzichunga amri za Allah Mtukufu. Na muogopeni Allah Mtukufu na mjue kwamba mtakutana na Yeye kwa kuhesabiwa Siku ya Kiyama. Na wape bishara njema Waumini, ewe Nabii, kwa yale ambayo yatawafurahisha na kuwapendeza ya malipo mema huko Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net