Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 222

Al-Baqara 2:222

البقرة

وَيَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَٱعْتَزِلُوا۟ ٱلنِّسَآءَ فِى ٱلْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ ٱللَّهُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلتَّوَّٰبِينَ وَيُحِبُّ ٱلْمُتَطَهِّرِينَ

Maana

Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie: hayo ni madhara. Basi jitengeni mbali na wanawake wakati wa hedhi, wala msiwakaribie mpaka wawe safi. Na wakishajisafisha, basi waendeeni namna alivyokuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu, na huwapenda wanaojisafisha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat'ahirike. Wakisha t'ahirika basi waendeeni alivyo kuamrisheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha. [222]

[222] Na wanakuuliza juu ya kuwaingilia wake zenu wakati wanapo kuwa na damu ya mwezi, hedhi. Waambie kuwa hedhi ni uchafu. Basi jizuieni kuwaingilia wakati wake mpaka wat'ahirike (wasafike). Wakit'ahirika basi ingianeni nao katika njia za maumbile. Na ikiwa mtu amefanya makosa katika haya, basi na atubu, na Mwenyezi Mungu anapenda waja wake wakithiri toba na usafi kutokana na uchafu. Ilimu ya kisasa zimethibitisha kuwa wakati wa hedhi yanaweza kuwa madhara kwa kuwa zalio huweza kupata maradhi pindi likiingiliwa na vidudu vya maradhi, ambavyo ni vyepesi kuingia wakati wa kuingiliana na mwanamume. Maradhi hayo huenda yakasababisha mwanamke asiweze kuzaa. Mwanamume naye huambukia maradhi hayo kutokana na mwanamke kwa kupitia njia za mkojo, na maradhi yakapanda juu mpaka mafigo yakaharibika, na kuathirika vyombo vya uzazi, na mwanamume naye akawa hawezi kutia mimba. Maradhi haya huleta machungu makubwa. Watu walikuwa hawajui, lakini Mwenyezi Mungu anajua kila kitu. Na mwanamke anapo kuwa na damu anakuwa hana raghba ya kuingiliwa, basi kumuingilia wakati huo huenda kukamletea hali ya nafsi mbaya na chuki kwa jambo hilo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wanakuuliza kuhusu hedhi, nayo ni damu inayotiririka kimaumbile kutoka kwenye uzao wa wanawake katika nyakati maalumu.Waambie, ewe Mtume, Hiyo hedhi ni udhia wenye manyezi unaomdhuru mwenye kuusongelea. Hivyo basi, jiepusheni kuwaingilia wanawake kwenye kipindi cha hedhi mpaka damu ikome. Damu ikomapo, na wakaoga, waingilieni kupitia pale pahali Alipowahalalishia Allah Mtukufu, napo ni tupu ya mbele siyo ya nyuma. Hakika Allah Mtukufu Anawapenda waja Wake wenye kutubia na kuomba msamaha kwa wingi na Anawapenda waja Wake wenye kujisafisha ambao hujitenga na maovu na uchafu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net