Al-Baqara 2:227
البقرةوَإِنْ عَزَمُوا۟ ٱلطَّلَـٰقَ فَإِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Na wakiazimia kuwapa talaka, basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mweye kujua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakiazimia kuwapa talaka basi, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mjuzi. [227]
[227] Na ikiwa hawakuwaingilia wake zao katika muda huu inakuwa hayo ni madhara kwa mwanamke. Basi hapana ila t'alaka tu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuzisikia yamini zao, na Mwenye kuzijua hali zao, na atawahisabu kwa hayo Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na iwapo wameamua kutaliki, kwa kuendelea kwao na kiapo chao na kuacha kufanya tendo la ndoa, Basi Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasikia maneno yao, ni Mjuzi wa Malengo yao, na Atawalipa kwayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net