Al-Baqara 2:220
البقرةفِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۗ وَيَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلْيَتَـٰمَىٰ ۖ قُلْ إِصْلَاحٌ لَّهُمْ خَيْرٌ ۖ وَإِن تُخَالِطُوهُمْ فَإِخْوَٰنُكُمْ ۚ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ ٱلْمُفْسِدَ مِنَ ٱلْمُصْلِحِ ۚ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ لَأَعْنَتَكُمْ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
Katika dunia na Akhera, na wanakuuliza juu ya mayatima. Sema: Kuwatengenezea ndio heri. Na mkichanganyika nao, basi ni ndugu zenu. Na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji. Na Mwenyezi Mungu angelipenda, angelikutieni katika ugumu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
--Katika mambo ya dunia na mambo ya Akhera. Na wanakuuliza juu ya mayatima. Sema: Kuwatengenezea ndio kheri. Na mkichanganyika nao basi ni ndugu zenu; na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji. Na Mwenyezi Mungu angeli penda angeli kutieni katika udhia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima. [220]
[220] Na wanakuuliza khabari ya mayatima: katika Uislamu inapasa watendejwe? Sema ni kheri yenu na yao kuwatendea wema. Wawekeni katika nyumba zenu pamoja nanyi, na changanyikeni nao kwa makusudio ya kheri si ya fisadi, kwani wao ni ndugu zenu duniani, wanahitaji kwenu mchanganyiko huu. Na Mwenyezi Mungu anamjua mharibifu na mtengenezaji katika nyinyi. Basi tahadharini! Na Mwenyezi Mungu angeli penda angeli kupeni taabu, akakulazimisheni kuwaangalia mayatima bila ya kuchanganyika nao, au angeli kuacheni bila ya kubainisha waajibu wanao pasa kutendewa. Kwa hivyo wangeli kulia kuchukia watu, na hayo yange pelekea kufisidika na kuleta shida kwa jamii zenu. Kwani kuwakahirisha mayatima na kuwadhili huwafanya wawachukie hao jamaa wawatendao vibaya. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kushinda katika amri yake, lakini naye ni Mwenye hikima halazimishi katika sharia ila lenye maslaha yenu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
duniani na Akhera. Na wanakuuliza, ewe Mtume, kuhusu mayatima, waamiliane nao vipi katika maisha yao na mali yao. Waambie, Kuwatengezea kwenu mambo yao ni bora. Basi, wafanyieni daima yanayowafaa wao zaidi.Na iwapo mtatangamana nao katika mambo ya maisha, basi wao ni ndugu zenu katika Dini. Na ni juu ya ndugu kuyalinda maslahi ya ndugu yake. Allah Mtukufu Anamjua mpotezaji wa mali ya mayatima na yule mwenye pupa la kuyahifadhi. Na lau Allah Mtukufu Angetaka, angewatia dhiki na mashaka kwa kuwaharamishia mtangamano. Hakika Allah Mtukufu ni Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwingi wa hekima katika uumbaji Wake, uendeshaji mambo Wake na upitishaji sheria Wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net