Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 218

Al-Baqara 2:218

البقرة

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ وَجَـٰهَدُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ أُو۟لَـٰٓئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ ٱللَّهِ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Hakika, wale walioamini, na wale waliohama na wakafanya juhudi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanaotarajia rehema za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale walio amini na wale walio hama na wakapigania Njia ya Mwenyezi Mungu, hao ndio wanao taraji rehema za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. [218]

[218] Wenye kuamini imani ya kweli hata wakahama kwa ajili ya kuinusuru Dini na kwa ajili ya Jihadi ili Dini ienee hao wanangojea thawabu kubwa za Mwenyezi Mungu. Na ikiwa wamefanya kasoro kitu basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, anasamehe dhambi, Mwenye kurehemu, anawarehemu waja wake kwa uwongofu na kuwalipa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wale ambao walimuamini Allah Mtukufu na Mtume wake na wakazitumia Sheria zake, wale walioyaacha Makaazi yao na wakapigana katika njia ya Allah Mtukufu, hao ni wenye kutaraji kupata fadhila za Allah Mtukufu na thawabu Zake. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyasamehe madhambi ya waja Wake Waumini, ni Mwenye kuwarehemu rehema kunjufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net