Al-Baqara 2:216
البقرةكُتِبَ عَلَيْكُمُ ٱلْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰٓ أَن تَكْرَهُوا۟ شَيْـًٔا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰٓ أَن تُحِبُّوا۟ شَيْـًٔا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinawachukiza. Lakini huenda mkachukia kitu, nacho ni heri kwenu. Na huenda mkapenda kitu, nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua, na nyinyi hamjui.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mmeandikiwa kupigana vita, navyo vinachusha kwenu. Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui. [216]
[216] Ikiwa kutoa kusaidia mayatima na masikini na wengineo ni kuhami jamii ya umma kwa ndani, kadhaalika kupigana vita ni kuuhami umma na adui wa nje. Kwa hivyo enyi Waislamu, mmelazimishwa kupigana vita kuhami Dini yenu, na kulinda nafsi zenu. Hakika hizo nafsi zenu kwa mujibu wa tabia zake zinachukia mno kupigana. Lakini huenda mkachukia kitu na ndani yake ipo kheri kwenu, na mkapenda kitu na ikawa ipo shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua maslaha yenu ambayo yamefichikana, na nyinyi hamyajui. Basi tendeni mlilo amrishwa kulitenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Amewafaradhia, enyi Waumini, kupigana na Makafiri, hali ya kuwa ni jambo lenye kuchukiwa na nyinyi kimaumbile, kwa uzito wake na hatari zake nyingi. Na huenda mkakichukia kitu nacho kwa uhakika wake ni kheri kwenu. Na huenda mkakipenda kitu kwa ajili ya raha na ladha za karibu zilizomo, nacho kwa uhakika wake ni shari kwenu. Allah Mtukufu Analijua lenye kheri kwenu, na nyinyi hamlijui hilo. Kwa hivyo harakisheni kupigana jihadi katika njia Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net