Al-Baqara 2:215
البقرةيَسْـَٔلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ ۖ قُلْ مَآ أَنفَقْتُم مِّنْ خَيْرٍ فَلِلْوَٰلِدَيْنِ وَٱلْأَقْرَبِينَ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ ۗ وَمَا تَفْعَلُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ
Wanakuuliza watoe nini? Sema: Chochote mnachotoa katika heri ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na msafiri. Na chochote mnachofanya katika heri, basi Mwenyezi Mungu kwa hakika anaijua vyema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanakuuliza watoe nini? Sema: Kheri mnayo itoa ni kwa ajili ya wazazi na jamaa na mayatima na masikini na wasafiri. Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua. [215]
[215] Waumini wanakuuliza mas-ala ya kutoa. Waambie: Kutoa iwe kutokana na mali mazuri, na wa kupewa ni wazazi wawili, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri aliye katikiwa na mali yake na watu wake. Na lolote katika vitendo vya kheri mlitendalo basi hakika Mwnyezi Mungu analijua na atakulipeni kwalo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wanakuuliza watu wako, ewe Nabii, «Ni kitu gani wakitoe, katika aina za mali zao, kujikurubisha kwa Allah Mtukufu? Na watoe kumpa nani?» Waambie, «Toeni kheri yoyote iliyo tahfifu kwenu katika aina za mali mazuri ya halali, na utoaji wenu uwe ni kwa wazazi wawili, walio karibu katika watu wenu na kizazi chenu, mayatima, mafukara na msafiri mwenye uhitaji aliye mbali na watu wake na mali yake. Na kheri yoyote mtakayoifanya, basi Allah Mtukufu ni mwenye kuijua».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net