Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 214

Al-Baqara 2:214

البقرة

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا۟ ٱلْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ ٱلَّذِينَ خَلَوْا۟ مِن قَبْلِكُم ۖ مَّسَّتْهُمُ ٱلْبَأْسَآءُ وَٱلضَّرَّآءُ وَزُلْزِلُوا۟ حَتَّىٰ يَقُولَ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ مَتَىٰ نَصْرُ ٱللَّهِ ۗ أَلَآ إِنَّ نَصْرَ ٱللَّهِ قَرِيبٌ

Maana

Ama mnadhani kuwa mtaingia Bustanini, ilhali bado hamjajiwa na mfano wa (yaliyowajia) wale waliopita kabla yenu? Uliwapata ufukara (shida) na maradhi, na wakatikiswa mpaka Mtume na walioamini pamoja naye wakasema: “Ni lini nusura ya Mwenyezi Mungu (itakuja)?” Jueni kuwa hakika nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu. [214]

[214] Hivyo mnadhani kuwa mtaingia Peponi kwa Uislamu wa kutamka tu bila ya kupatikana na masaibu mfano wa masaibu yaliyo wasibu walio kuwa kabla yenu? Hao walipata shida na mashaka na mateso, wakatikiswa mpaka ikafika hadi ya kuwa Mtume wao mwenyewe kusema, na wao wakasema vile vile pamoja naye: Lini itakuja nusura ya Mwenyezi Mungu? Mola wao Mlezi basi anawahakikishia kwa ahadi yake kwa kuwajibu kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwani mlidhani, enyi Waumini, kwamba mtaingia Peponi, na bado haijawapata mitihani kama ile iliyowapata Waumini waliopita kabla yenu: ya ufukara, maradhi, kitisho na babaiko, na wakatikiswa kwa aina nyingi za misukosuko ya kutisha, mpaka akasema Mtume wao na Waumini pamoja naye, kwa njia ya kuharakisha nusura ya Allah Mtukufu, «Ni lini hiyo nusura ya Allah Mtukufu?» Jueni kwamba nusura ya Allah Mtukufu iko karibu na Waumini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net