Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 198

Al-Baqara 2:198

البقرة

لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا۟ فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ ۚ فَإِذَآ أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَـٰتٍ فَٱذْكُرُوا۟ ٱللَّهَ عِندَ ٱلْمَشْعَرِ ٱلْحَرَامِ ۖ وَٱذْكُرُوهُ كَمَا هَدَىٰكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِۦ لَمِنَ ٱلضَّآلِّينَ

Maana

Hakuna ubaya wowote juu yenu kutafuta fadhila kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi mtakapomiminika kutoka 'Arafat, mtajeni Mwenyezi Mungu katika Mash'aril Haram (eneo takatifu). Na mtajeni kama alivyowaongoa, ijapokuwa kabla ya hilo mlikuwa miongoni mwa waliopotea.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Si vibaya kwenu kuitafuta fadhila ya Mola wenu Mlezi. Na mtakapo miminika kutoka A'rafat mtajeni Mwenyezi Mungu penye Masha'ril Haram. Na mkumbukeni kama alivyo kuongoeni, ijapo kuwa zamani mlikuwa miongoni mwa walio potea. [198]

[198] Na walikuwako miongoni mwenu ambao wakiona vibaya kufanya biashara na kutafuta riziki wakati wa msimu wa Hija. Basi mnaambiwa kuwa hapana ubaya kwenu hayo, bali mnaweza kuchuma maisha kwa njia ziliyo ruhusiwa na sharia, na mtafute fadhila na neema za Mwenyezi Mungu. Wakitoka Mahujaji A'rafat baada ya kusimama huko, na wakafika Muzdalifa katika mkesha wa Idi ya Kuchinja, wamtaje Mwenyezi Mungu hapo Masha'ril Haram, napo ndipo kwenye kilima cha Muzdalifa, kwa kusoma Tahlili na kuitikia Labbaika na kusoma Takbir. Na wamtukuze Mwenyezi Mungu wakimhimidi na kumshukuru kwa vile alivyo waongoa kwenye Dini ya Haki na ibada iliyo nyooka katika Hija na Umra, na ilhali kabla ya hapo walikuwa katika walio potea njia ya uwongofu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapana ubaya wowote kwenu kutafuta riziki itokayo kwa Mola wenu, kwa kupata faida ya biashara, ndani ya siku za Hija.Basi mtakapo kuondoka, baada ya kuchwa jua, mkirejea kutoka Arafa- napo ni pahali ambapo Mahujaji husimama siku ya tisa ya Mfungotatu-, mtajeni Allah Mtukufu kwa kuleta Tasbihi, Talbiyah(Labbaika Allãhumma labbaika..) na dua katika sehemu tukufu ya Al-Mash՚ar al-Harãm: Muzdalifa. Na mumtaje Allah Mtukufu kwa njia ya kisawa Aliyowaongoza nayo. Na mlikuwa kabla ya uongofu huo mko katika upotevu, hamuijui haki.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net