Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 183

Al-Baqara 2:183

البقرة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كُتِبَ عَلَيْكُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

Maana

Enyi mlioamini! Mmeandikiwa Saumu, kama walivyoandikiwa (watu) waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu. [183]

[183] Na kama tulivyo kuwekeeni sharia za Kisasi na Wasiya kwa ajili ya maslaha ya jamii zenu, na kuhifadhi mambo ya ukoo, kadhaalika tumeweka sharia za Saumu ili kuzitengeneza nafsi zenu, ziweze kujikinga na matamanio, na kukutukuzeni kuliko wanyama walio baki wanao fuata hisiya za matamanio yao tu. Na huku kufaridhishwa Saumu ni kama walivyo faridhishwa kaumu zilizo tangulia. Basi msilione kuwa ni jambo zito mno hili, kwani watu wote walilazimishwa haya. Kulazimishwa Saumu ni kwa ajili ipate kuleleka roho ya uchamngu, na ili muwe watu madhubuti, na nafsi zenu ziongoke sawa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mumemuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mukaifuata Sheria Yake kivitendo, Allah Mtukufu Amewafaradhia kufunga, kama Alivyowafaradhia ummah waliokuweko kabla yenu, ili mupate kumcha Mola wenu na kuweka kinga kati yenu na maasia, kwa kumtii na kumuabudu Peke Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net