Al-Baqara 2:182
البقرةفَمَنْ خَافَ مِن مُّوصٍ جَنَفًا أَوْ إِثْمًا فَأَصْلَحَ بَيْنَهُمْ فَلَآ إِثْمَ عَلَيْهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Na mwenye kumhofia muusiaji kwenda kombo au kupata dhambi, na akasuluhisha baina yao, basi hakuna dhambi yoyote juu yake. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na mwenye kumkhofia muusiaji kwenda kombo au kupata dhambi akasuluhisha baina yao, basi hatakuwa na dhambi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu. [182]
[182] Ama ikiwa wasiya umeacha haki na njia iliyo sawa tuliyo kwisha ibainisha, kwa mwenye kufanya wasiya kumharimisha fakiri akampa tajiri, akawawacha jamaa zake akawapa mafakiri wasio rithi watu mbali, basi mwenye kwenda mwendo wa kheri akamrejeza mwenye kufanya wasiya ende sawa, basi hapana dhambi kwa kuugeuza wasiya kwa namna hiyo. Na Mwenyezi Mungu hamchukulii kitu kwa hayo, kwani Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi yoyote atakayejua kuwa mwenye kuusia amepinduka, kwa kuiacha haki katika wasia wake kwa njia ya kukosea au kukusudia, akamnasihi mtoaji wasia, wakati wa kutoa wasia, afanye uadilifu, na iwapo hilo halikuwa akaleta upatanishi kati ya pande zinazohusika kwa kugeuza wasia ili ulingane na Sheria, basi atakuwa hana dhambi katika kupatanisha huku. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa kuwasamehe waja wake, ni Mwenye huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net