Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 181

Al-Baqara 2:181

البقرة

فَمَنۢ بَدَّلَهُۥ بَعْدَ مَا سَمِعَهُۥ فَإِنَّمَآ إِثْمُهُۥ عَلَى ٱلَّذِينَ يُبَدِّلُونَهُۥٓ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Maana

Na atakayeibadilisha (wasia) baada ya kuisikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakaoibadilisha; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na atakaye ubadilisha wasia baada ya kuusikia, basi dhambi yake ni juu ya wale watakao ubadilisha; hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua. [181]

[181] Ukitoka wasiya basi huo ni haki iliyo waajibu, haijuzu kuugeuza na kuubadilisha ila ikiwa wasiya huo umeacha uadilifu. Mwenye kubadilisha haki akageuza wasiya muadilifu ulio sawa baada ya kujua hukumu hii basi huyo amepanda madhambi yatakayo mletea adhabu. Mwenye kuusia hana kosa kwa yatakayo tokea baada yake, wala hakudhani kuwa atakuwapo atakaye fanya hayo, wala yeye hapatilizwi kwa hayo. Mwenyezi Mungu, hakika, ni Mwenye kusikia na kujua, wala hapana linalo fichikana kwake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yule atakaye kuubadilisha wasia wa maiti baada ya kuusikia kutoka kwake kabla hajafariki, dhambi litakuwa ni la yule aliyebadilisha na kugeuza. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye kuusikia wasia wenu na maneno yenu, ni Mjuzi zaidi wa yale yanayofichwa na nyoyo zenu kuhusu kuelekea upande wa haki na uadilifu au ujeuri na udhalimu, na Atawalipa kwa hilo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net