Al-Baqara 2:180
البقرةكُتِبَ عَلَيْكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ ٱلْمَوْتُ إِن تَرَكَ خَيْرًا ٱلْوَصِيَّةُ لِلْوَٰلِدَيْنِ وَٱلْأَقْرَبِينَ بِٱلْمَعْرُوفِ ۖ حَقًّا عَلَى ٱلْمُتَّقِينَ
Mmeandikiwa mmoja wenu anapofikwa na mauti, kama ataacha heri (yaani mali), afanye wasia kwa wazazi wake wawili, na jamaa zake kwa wema. Ni haki juu ya wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mmeandikiwa -- mmoja wenu anapo fikwa na mauti, kama akiacha mali -- afanye wasia kwa wazazi wake na jamaa zake kwa namna nzuri inayo pendeza. Ni waajibu haya kwa wachamngu. [180]
[180] Kama tulivyo weka sharia ya kisasi kwa maslaha ya umma na kuhifadhi jamii, vile vile tumeleta sharia ya maslaha ya ukoo na kuulinda, nayo ni Sharia ya Wasiya. Basi mwenye kuona kuwa amekabiliwa na mauti naye akawa na mali basi yatatikana awawekee katika mali yake fungu la wazazi wake na jamaa zake, wale jamaa ambao hawamrithi. Katika hayo afuate mwendo unao pendeza na unakubaliwa na wenye akili. Asiwe akampa tajiri na akamwacha fakiri, bali amfadhilishe yule mwenye haja zaidi, wala asiweke sawa ila wale wenye pato sawa. Na faridha hiyo ni haki iliyo mwajibikia mwenye kupenda uchamngu na kufuata amri za Dini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Amewafaradhia nyinyi, iwapo mmoja wenu zimedhihiri kwake alama za mauti na vitangulizi vyake, akiwa ameacha mali, atoe wasia wa sehemu ya mali yake iyende kwa wazazi wake wawili na jamaa zake walio karibu naye, pamoja na kuchunga uadilifu, asimuache masikini na akatoa wasia wake kwa tajiri, wala wasia wake usizidi thuluthi ya mali. Hiyo ni haki thabiti ambayo wenye kumcha Allah Mtukufu waitenda. Hii ilikuwa kabla ya kuteremka zile aya ambazo Allah Mtukufu aliweka fungu la kila mrithi.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net