Al-Baqara 2:179
البقرةوَلَكُمْ فِى ٱلْقِصَاصِ حَيَوٰةٌ يَـٰٓأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
Mtakuwa na uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili mpate kuwa wacha Mungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike. [179]
[179] Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu kwenu ni kubwa kwa hii hukumu ya kisasi. Kwa fadhila ya kisasi jamii yenu ina hakika kupata maisha ya amani na salama. Haya ni kwa kuwa mwenye kutaka kuuwa akijua kuwa naye atauwawa atajizuia kutenda alilo kusudia. Kwa hivyo yeye na yule ambaye angeli uwawa wanahifadhika. Lakini ikiwa kama ilivyo kuwa zama za ujahili akiuliwa mkuu kwa kuuliwa mtu mdogo, na asiye na kosa badala ya mwenye makosa - hapo inakuwa ni kuzua fitna, na kuondoka utulivu na amani. Wenye akili nawazingatie faida ya sharia ya kisasi. Hayo yatawapelekea watambue upole wa Mwenyezi Mungu kwao kuendea njia ya uchamngu, na kuzifuata amri za Mwenyezi Mungu Subhanahu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hakika katika kuwekwa sheria ya kisasi na utekelezaji wake kwa kutarajia kufikia uchaji Allah Mtukufu na kumuogopa kwa kumtii daima, kuna maisha ya amani kwenu, enyi wenye akili timamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net